Swahiliksi: Mikä on Kodin ja Koulun Päivä?

Siku ya Nyumbani na Shuleni ni gani?   

Ukipata mwaliko wa tukio hili kutoka shuleni, ni muhimu kuhudhuria!

Shule nyingi za Kifini huandaa Siku ya Nyumbani na Shuleni kila mwaka (Kodin ja Koulun Päivä). Ni tukio lenye utulivu na lisilo rasmi ambapo wazazi wanaweza kufahamu shule ya mtoto wao, kukutana na walimu na wafanyakazi wengine, na wazazi wengine na watoto. Katika Siku ya Nyumbani na Shuleni unaweza kuona wapi na ni nani wanaosoma na watoto wako.  

Shule nyingi hufanya tukio hilo mwishoni mwa mwezi Septemba, lakini linaweza pia kuandaliwa katika nyakati nyingine. Huenda tukio hilo likafanyika katika siku ya shule, jioni, au mwishoni mwa wiki.  

Baadhi ya shule hupanga programu ya tukio hilo, kwa mfano maonyesho ya densi, michezo ya pamoja na kucheza, kusoma, safari ya kwenda msituni au hata warsha za urekebishaji wa baiskeli. Baadhi yao hutoa kahawa na pengine kitu cha kula. Katika baadhi ya shule, unaweza kuangalia madarasa. Mwaliko utakuambia kitakachofanywa shuleni kwako na wakati gani.   

Ukipata mwaliko wa tukio, tunakuhimiza sana uhudhurie. Unaweza kushiriki hata ikiwa huzungumzi Kifini/Kiswidi. Ukipata taarifa kwa wakati, unaweza kuomba likizo usije kazini. Nchini Ufini, inaaminika kwamba ni vizuri kwa wazazi kushiriki katika matukio yaliyoandaliwa na shule.  

Ni muhimu kwa wazazi na walimu kujuana na kushirikiana. Siku ya Nyumbani na Shuleni ni njia rahisi ya kujuana. Ni rahisi kuchangamana na wengine mkikutana ana kwa ana. Ni muhimu kwa watoto kuwahusisha wazazi wao!  

Shule nyingi zina vyama vya wazazi. Katika Siku ya Nyumbani na Shuleni, unaweza kuuliza iwapo kuna chama kama hiyo katika shule ya mtoto wako na kile anachofanya na jinsi unavyoweza kushiriki katika shughuli hizo. Wazazi wote mnakaribishwa kushiriki katika shughuli za chama cha wazazi! Vyama vingi vya wazazi hupanga tukio la Siku ya Nyumbani na Shuleni pamoja na shule.

www.kodinjakoulunpaiva.fi